Karibu DSN TECHNOLOGY!
Kabla hujaendelea kusoma, chukua maji ya baridi au kahawa (kulingana na hali ya hewa), kisha kaa vizuri... maana kama kazi yako ipo kwenye hii listi, usishtuke – tupo pamoja. Dunia inabadilika kasi kuliko supu ya mama inapowekwa kwenye friji, na ajira nazo hazipo salama.

Sasa basi, hebu tuone hizi kazi 21 ambazo ziko kwenye ICU ya mabadiliko ya teknolojia – nyingine zinahema kwa mashine, nyingine zimeshapoteza fahamu, na nyingine zinasubiri tu "pull the plug."

1. Dereva wa Taxi/Mpiga Debe wa Daladala

Kama umezoea kusema "Kariakoo wawili tu!" jua kuna siku hiyo sauti haitasikika. Magari yanayojiendesha (self-driving cars) yanaingiza gear tayari. Uber na Waymo wameanza kuwasahau madereva kabisaaa.

2. Cashier wa Supermarket

ATM ilianza, sasa ni self-checkout machines. Hata mama lishe akipewa mashine, atakuambia, "weka mwenyewe, kaka."

3. Mhasibu wa Kawaida (ambaye hajui tech)

Zamani kulikuwa na watu wanapiga hesabu kwa karatasi na calculator ya sauti kubwa. Siku hizi, programu kama QuickBooks, Xero, na AI zinawageuza wasiojifunza kuwa wasimulizi wa hadithi za "nilivyokuwa nikipiga hesabu".

4. Wakala wa Safari (Travel Agent)

Kama bado unawaambia watu, "Nitakutafutia tiketi ya ndege," basi ujue Google, Booking.com, na apps nyingine zinakutazama kama unavyoangalia DVD player mwaka 2025.

5. Fundi wa Kutengeneza VCR au Redio za Teti

Sema kweli, lini mara ya mwisho ulitumia VCR? Ndio... tulia.

6. Mkusanyaji wa Takwimu za Mikono (Manual Data Entry Clerk)

Kazi ya kuandika data kwa mikono? AI na OCR zimeshachukua hiyo. Mpaka kesho kuna bots zinaandika haraka kuliko mtu aliyepewa mshahara wa mwezi.

7. Askari Trafiki (ambao hawana kamera)

Kamera za barabarani na AI traffic control zinaonekana kuwa na subira kuliko binadamu – na hazihitaji chai!

8. Watangazaji wa Habari wa Kawaida (TV)

YouTube, TikTok, na Podcasts vimefanya kila mtu kuwa "mtangazaji" – bila suit wala makeup ya studio.

9. Mafundi wa Kamera za Siku za Kale

Kama bado unarekebisha kamera za film, labda unahitaji kubadilisha "lens" ya maisha.

10. Wachapishaji wa Magazeti

Digital news is king. Printing ni gharama, digital ni 'tap and go'. Kama bado unasubiria gazeti la kesho, basi pole!

11. Wahudumu wa Simu (Call Center ya Sauti tu)

Bots wenye sauti tamu (mara nyingine kuliko mpenzi wako) wanaweza kujibu simu, kuelekeza huduma, na hata kukupa pole kwa 'delay.'

12. Walinzi wa Ofisi (ambao hawajui CCTV/Tech)

Robots wa usalama na AI camera ziko kazini usiku na mchana – hazichoki, hazilali, na haziombi ruhusa.

13. Karani wa Ofisi

Mtu wa kupanga mafaili, kutoa kopi, kuchukua simu? Google Calendar, AI Assistant na Email Automation wanapiga kazi hizo bure!

14. Fundi wa Mashine za Kuandika

Ndiyo, kuna mtu bado anajua kutumia typewriter. Lakini pole yake, watoto wa Gen Z hawajui hata hiyo ni nini.

15. Mwalimu wa Kawaida (ambaye hatumii teknolojia)

Mwalimu asiyejua Zoom, Google Classroom, au hata Kahoot! ataachwa nyuma kama vitenge vya enzi za Nyerere.

16. Wahudumu wa Mabenki (ambao hawajui digital banking)

Kazi ya kukupa 'balance inquiry' ilishaondoka. Apps ziko kazini saa 24, hata Jumapili.

17. Watu wa Kutangaza Ajira kwa Mabango

LinkedIn, Glassdoor, na AI recruitment tools zimewafanya watu wa "Kuna kazi pale Buguruni" kukosa wasikilizaji.

18. Wasanii wa Karatasi (Graphic Designers wa 'Manual')

Kama bado unatumia "ruler na penseli" kuchora logos, pole. Figma, Canva na Adobe AI ziko kwenye ligi nyingine.

19. Wahifadhi wa Maktaba (ambao hawajakumbatia digital)

E-books, audio books, na online libraries zinafanya kazi ya kurudisha kitabu cha mkopo kuwa historia.

20. Mkalimani wa Lugha Maarufu (kama Kiingereza-Kiswahili)

Google Translate, DeepL, na AI voice translators wanapiga kazi hadi kwenye simu yako ya tochi!

21. Mhariri wa Video Anayetumia Tools za Kale

Kama bado unakata video kwa "Windows Movie Maker" au software ya 2005, jua AI video editors zinaweza kukuchomeka background, kurekebisha sauti, na kuunganisha video kwa dakika chache.

NAJUA UNAJIULIZA – Sasa Nifanyeje?

Kwanza, usihofu. Kama kazi yako iko hapo juu, hii si mwisho wako – ni mwanzo wa mabadiliko.
Jifunze, jiongeze, jikite kwenye teknolojia. Kama huwezi kushindana na AI, basi ishirikishe.
Unakumbuka Nokia? Ilisema "Connecting People" lakini ilipojilaza tu, simu janja zikaitupa nje.

Je, Ungependa Kujifunza Skills Zitakazokuweka Salama?

Endelea kutembelea DSN TECHNOLOGY – tunakuletea tips, tutorials, na mbinu za kutengeneza ajira hata AI ikiamka na hasira!

Usisahau kushare hii post kwa watu wako – usiwacheke peke yako.

Jiunge na Group Letu