Author: Danieli Emannueli – DSN TECHNOLOGY
Kwanza kabisa... usije hapa na akili ya weekend, hapa tunazungumza kuhusu Followers siyo kuhusu status za "feeling blessed". Hii post ni kwa wale wanaotaka matokeo, siyo wale wanaoweka picha ya ugali na kuandika "Guess my dinner".
Hebu Tuanze na Ukweli Mchungu
Ukweli ni huu: Facebook haitoi followers kwa huruma, wala kwa sababu una jina zuri kama "Musa wa TikTok". Huko ni kujidanganya. Hivi unajua kuna watu wanapiga 5,000+ followers kwa siku moja, wakati wewe bado unawangoja ndugu zako wa mtaa waku-follow? Acha! Leo nakupa mbinu mpya – yaani FRESH kutoka jikoni – na siyo zile za mwaka 2017 za "like for like".
Sasa Sikiliza Hii SIRI KALI
> MBINU: Tumia Kisasi cha CONTENT Inayochoma!
Usitake kujifanya Mwana-Mtume Facebook, watu hawataki maombi kila post. Watu wanataka content yenye utamu, ukali, ucheshi, kejeli kidogo, na ile feeling ya "hii lazima ni-tag mtu." Hapo ndipo utashuhudia followers wakijaa kama watu kwenye daladala ya asubuhi.
Hapa Ndio Siri Ipo:
- Andika Post za "UCHUNGU wa MAISHA" lakini kwa UTANI.
Mfano:
"Ushawahi kuomba 5k ukajibiwa na emoji ya sad face?"
- Tengeneza VIDEO za SECONDS 30 ZENYE MADONGO.
Kama video inaongelea watu wanaojidai matajiri halafu wako kwa wifi ya kanisa – Trust me, watu wata-share, wata-comment "@Jane ni wewe" na hapo ndipo Facebook inakutangaza. - Tumia maudhui ya TREND kwa STAILI YAKO.
Usikopi content kama unaiba password ya ex. Chukua trend, ipike na chumvi zako. Mfano: Kama watu wanaongelea "Wivu wa mapenzi", wewe ongelea "Wivu wa hotspot" – funny, unique, relatable! - Jiunge na MAGROUP yenye MISHENI.
Kuna magroup Facebook yenye watu active kuliko hata wazazi wa WhatsApp. Ukiweka post kali humo, feedback ni faster kuliko hata internet ya Zuku.
Jambo la KUSHANGAZA
Unajua unaweza kupata 5,000 followers bila hata kutumia boost ya Tsh 1?
YES! Ila tatizo lako unataka followers wa bei rahisi kama socks za Kariakoo.
BONUS YA WATAKAOCHANGAMKIA HII FOMU
Ikiwa unataka kutumia hii mbinu halafu ukae kimya kama uko exile – pole zako. Hii mbinu inahitaji:
- Kuwa active (Siyo mtu wa post moja kwa wiki)
- Kujibu comments (acha kiburi, hujaomoka bado)
- Ku-follow watu wengine pia (siyo dhambi)
Mwisho wa Mchezo
Kama umesoma hadi hapa, basi tayari una point za kuanza. Na kama bado hautapata followers 5K kwa siku, basi ni aidha:
- Unapost picha za chai kila siku
- Unasema "mambo" bila content
- Au uko tu stubborn – unadhani wenye followers wengi wachawi
Ni mimi tena Danieli Emannueli kutoka DSN TECHNOLOGY, ambapo hatufundishi tu tech – tunachoma hadi ego za wanaodharau content. Ukitaka part 2, sema "TUPIE" kwenye comments. Usitegemee miujiza kama bado unatumia status ya "Don't disturb".
Usisahau kushare kwa wale marafiki zako wanaomba followers kama wanaomba vocha.
#DSNTECHNOLOGY | #FollowHustle | #ContentNiSilaha | #UsiweMtakatifuKwenyeFacebook